Rais Magufuli leo Septemba 5 akiwa kwenye kampeni Mara amewapongeza Madaraka na Makongoro Nyerere kwa kudumisha Demokrasia licha ya kutokupitishwa na wajumbe.
"Lakini nawapongeza hata watoto wako kwa kudumisha demokrasia ya nchi hii waliomba ubunge Butiama kule mmoja akapata kura 5 mwingine kura 2, wajumbe jamani nyinyi wajumbe,wajumbe ni hatari sana ila hawakulalamika wala kuhama chama", amesema Dkt. Magufuli.
Aidha Rais Magufuli alimshukuru Mama Maria kwa faraja na maneno mazuri juu ya kuumwa kwa mama yake na ujio wake leo kwa ajili ya kumuombea kura kwa wananchi wa Mara.
"Leo umeamua kuja hapa kuniombea kura ninajua wenzetu wanaotafuta kura hujawahi kuguswa kuja kuwaombea kura umeguswa kuja kuniombe kura mimi pamoja na wabunge na madiwani wa CCM asante sana mama na Mungu akujalie", amesema.