Watoto 10 wamepoteza maisha baada ya Shule ya Msingi Byamungu Islamic iliyoko Kata ya Itera wilayani Kyerwa mkoani Kagera, kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Septemba 14, 2020. Mkuu wa Wilaya hiyo Rashid Mwaimu amethibitisha.

Jumla ya wanafunzi 74 walikuwepo kwenye bweni hilo ambalo chanzo cha moto hakijajulikana na RC wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesitisha shughuli za malazi katika shule hiyo kwa muda.

The post KAGERA: Wanafunzi 10 wapoteza maisha baada ya bweni la shule kuwaka moto (+Video) appeared first on Bongo5.com.