“Sasa hivi Makao Makuu ya Nchi yetu yapo Dodoma na mimi mwenyewe ninakaa Dodoma, sitashindwa kufanya maendeleo katika Wilaya ya Bahi kwa sababu Bahi na Dodoma ni pua na mdomo,nawahakikishia sitawaangusha, tumetoka mbali”
“Kwenye miaka 5 tutaendeleza jitihada kwa kukamilisha pale tulipoishia, tutaendelea na ujenzi wa vituo vingine vya afya, tutaendelea kuboresha elimu bila malipo, tutahakikisha tunafikisha umeme kwenye Vijiji 16 vilivyobaki kwenye Wilaya hii ya Bahi”
“Tumejenga Hospitali ya Wilaya ambayo ujenzi wake umefikia 95% kwa Tsh Bilioni 1.8, nataka hii Hospitali ya Wilaya imalizike haraka ili wananchi wa Bahi wawe wanatibiwa hapahapa na ndiyo maana ninawaomba mnipe kura nikamalizie kiporo kilichobaki”
The post JPM: Tutaendeleza jitihada kwa kukamilisha pale tulipoishia, tutajenga vituo vingine vya afya na kuboresha elimu bila malipo (+Video) appeared first on Bongo5.com.