Kampuni ya Tibasima imezindua jarida lake jipya la vibonzo @gumzoeastafrica ambalo litakuwa linapatikana mitandaoni.
Akiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Gumzo, Marco amesema amelileta jarida hilo jipya baada ya kuona kuna mahitaji ya jarida la vibonzo baada ya magazeti kama Sani na mengine ambayo yalikuwa yanafanya hivyo kupotea sokoni.
Marco ambaye alifanya kazi Sani kwa miaka mingi, amesema ujio wa jarida hilo utakata kiu kwa mashabiki ambao walikuwa wanayapenda.
The post Jarida la vibonzo la Gumzo lazinduliwa Dar (Video) appeared first on Bongo5.com.