Mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM, Dkt John Pombe Magufuli, leo Septemba 20, 2020 ameendelea na kampeni zake akiwa Uvinza aliposimama kuzungumza na wananchi, Magufuli amempigia simu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Selemani Jafo na kumtaka apeleke pesa Bilioni tano kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Uvinza yenye urefu wa KM 10.

“Mimi Niko Uvinza, tulitoa ahadi kutengeneza KM 10 kwenda Uvinza Mjini, TARURA wanatengeneza KM 1 tu, nimeshatoa maagizo TARURA uwaletee Bilioni 5 wamalize KM zote 10 za kwenda Uvinza, Sawa Waziri.”

Imeandikwa na Hamza Fumo, Instagram @fumop255

 

The post Dkt Magufuli mgombea Urais CCM ampigia simu ‘Laivu’ Waziri Jafo – Uwaletee Bilioni 5  (+Video) appeared first on Bongo5.com.