Je Ikulu ya Urusi itaweza kuifanya Marekani kuwa Bora zaidi ? Beijing inampendelea Joe Biden?. Maswali haya yako kwenye vichwa vya intelijensia ya Marekani wakati nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi mwezi Novemba.
Tathmini ya maafisa wa juu inaonya kwamba, nchi za kigeni zenye nguvu zitatumia uwezo wake wote kujaribu kuwa na ushawishi katika uchaguzi wa Marekani, na kuzungumzia hasa Urusi, china na Iran.
Aidha, nchi hizo pia kila moja inamalengo yake na uwezo wake binafsi.
Tathmini hizo zinafanyiwa uchuguzi pia na hivi karibuni mfichuzi alidai kwamba alitakiwa kupuuzilia mbali tishio linalotokana na Urusi kwasababu kunafanya Rais kuonekana mtu mbaya.
Hivyo basi ikiwa na zaidi kidogo tu ya mwezi mmoja kabla ya Marekani kufanya uchaguzi je ni kipi ambacho raia wa nchi hiyo wanastahili kufahamu?
Urusi
Je shirika la Ujasusi la Marekani linasema nini?
Kama ambavyo inafahamika, Urusi ilikuwa na jukumu katika uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 na matokeo yake.
Kwa ufupi, Shirika la Ujasusi la Marekani linaamini kwamba Urusi ilijaribu kushawishi uamuzi wa wapiga kura kumpendelea Donald Trump, na kugusia mikutano kati ya timu yake na maafisa wa Urusi, na kufanyika kwa shambulio la kimtandao dhidi ya mpinzani wake wakati huo Hillary Clinton na Wanademocrats.
Mwezi uliopiTa, jopo la seneti la Republican liliunga mkono mtazamo kwamba Urusi ilitaka Trump aibuke na ushindi na kuhitimisha kwamba kampeni yake ni rahisi kulengwa na nchi za kigeni lakini wakatupilia mbali madai ya njama ya kihalifu.
Kwa mwaka 2020, mbadilishano wa Hillary Clinton na Joe Biden. Katika tathimini yake iliyokuwa ikitarajiwa kusomwa na Umma wa Marekani, Mkuu wa kituo cha usalama na kupambana na ujasusi (NCSC) William Evanina amesema kuwa Urusi ilikuwa ”ikitumia hatua mbalimbali kuonesha dharau kwa Makamu wa rais wa zamani, Joe Biden”.
Urusi wakati wote imekana kuingilia chaguzi za nje.
Mapema mwaka huu msemaji wa Ikulu ya Urusi aliita shutuma za kuingilia chaguzi za nje kuwa ”matangazo ya wazimu” ambayo hayakuwa na uhusiano wowote na ukweli”.
Kama Urusi inataka muhula wa pili kwa Rais Trump au la, maoni mengine mara nyingi yanaoneshwa na wachambuzi ni kwamba nchi hiyo ina lengo pana la kuwatuliza wapinzani kwa kueneza mkanganyiko.
Kwa mfano mwaka huu waraka wa Umoja wa Ulaya ulidai kuwa kulikuwa na kampeni ya Urusi kutoa taarifa ghushi kuhusu virusi vya corona ili iwe vigumu kwa EU kuwasiliana kuhusu kushughulika na janga hilo.
Hata hivyo, Urusi ilisema kuwa madai hayo hayana msingi.
Wagombea wamesema nini?
Joe Biden hivi karibuni alionya kuwa ”kutakuwa na malipo” ikiwa Urusi itaendelea kuingilia, akiiita ”mpinzani” wa Marekani.
Baada ya mkutano wa kilele wa 2018 na Vladimir Putin, aliulizwa ikiwa anaamini jamii ya kijasusi ya Marekani au rais wa Urusi kuhusu madai hayo Bw. Trump alisema: “Rais Putin anasema sio Urusi. Sioni sababu yoyote kwanini itakuwa.” Baadaye alisema alikuwa amekosea kusema.
CHINA
Je shirika la Ujasusi la Marekani linasema nini?
Sauti za watu maarufu katika utawala wa Trump zimesema kuwa ni China, ambayo imekuwa tishio kubwa mwaka huu.
”Nimeona intelijensia. Hilo ndio hitimisho nililonalo,” Mwanasheria mkuu William Barr alisema. Adam Schiff wa Democrat, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya intelijensia ya bunge la wawakilishi, alimtuhumu Bwana Barr kwa ”kusema uongo wa dhahiri”
Katika tathmini yake, Bwana Evanina alisema intelijensia ya Marekani inaamini “China inapendelea kuwa Rais Trump – ambaye Beijing inamchukulia kama mtu asiyetabirika – asipate ushindi tena”.
“China inapanua juhudi zake za ushawishi kuunda mazingira ya sera huko Marekani, kushinikiza wanasiasa wanaowaona wako kinyume na masilahi ya China” alisema.
Nia inaweza kuwa zaidi na kutangaza maoni ya China.
Hivi karibuni Facebook ilifunga mtandao wa akaunti zilizounganishwa na China ambazo nyingi ziliunga mkono China, kama vile maslahi yake katika Bahari ya Kusini ya China.
China imekanusha kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine, ikisema ”haina mpango wa kufanya hivyo”.
Wagombea wanasema nini?
Mwezi huu, Rais Trump alirudia kuchapisha makala kwenye mtandao wa Twitter kutoka kwenye tovuti ya Breitbart yenye kichwa cha habari ” China inaonekana kumpendelea Joe Biden kwenye uchaguzi wa urais”.
“Hakika wanamtaka Biden. Nimechukua mabilioni ya dola kutoka China na kuwapa wakulima wetu na Hazina ya Marekani. China ingeimiliki Marekani ikiwa Biden na Hunter wangeingia!” Bwana Trump aliandika, akimaanisha Hunter mtoto wa Joe Biden.
Uhusiano wa Marekani na China ni hafifu, na mgogoro kuhusu kila kitu kutoka masuala ya virusi vya corona hadi China kuweka sheria yenye utata ya usalama huko Hong Kong.
Joe Biden ametafuta kujitetea dhidi ya tuhuma kutoka kwa Rais Trump kuwa yeye ni mpole kwa China, akiahidi kuwa “thabiti” kuhusu haki za binadamu na masuala mengine.
Democrats ingawa wanasema kuwa linapokuja suala la uchaguzi angalau, ni Urusi ambayo inakuwa na ukaidi zaidi.
IRAN
Je shirika la Ujasusi la Marekani linasema nini?
Katika taarifa yake Bw. Evanina anasema kuwa Tehran inapinga muhula mwingine wa Rais Trump, ambapo inaamini kuwa kuwepo kwake kutasababisha ”muendelezo wa Shinikizo la Marekani kwa Iran katika jitihada za kuchochea mabadiliko ya utawala”.
Juhudi za Iran, anasema, zitaweka angalizo kwa “ushawishi wa kwenye mtandao, kama vile kusambaza taarifa zisizo na ukweli kwenye mitandao ya kijamii na kueneza maudhui ya kuipinga Marekani”.
Akiunga mkono madai ya Intelijensia ya marekani, Kampuni ya Microsoft ilisema wavamizi wenye kuhusishwa na urusi, China na Iran wanajaribu kupeleleza masuala ya msingi katika uchaguzi wa Marekani.
Upande wa Iran, ilisema kwamba kundi la Iran la Phosphorus lilishindwa kufikia akaunti za Ikulu ya Marekani na wafanyakazi wa kampeni ya Bwana Trump kati ya Mei na Juni mwaka huu.
Waziri wa mambo ya nje wa Iran aliitaja ripoti ya kampuni ya Microsoft kama “upuuzi mtupu”. “Iran haihangaiki na suala la ni nani atakayekuwa rais wa Marekani,” amesema Saeed Khatibzadeh.
Wagombea wanasema nini?
Iran haijatokea kuwa na ushawishi mkubwa katika uchaguzi wa Marekani ikilinganishwa na Urusi na China, zote kwa misingi ya uwezekano wa ushawishi wake au kisera.
Rais Trump ameendeleza sera yake kali dhidi ya Iran kwa kujiondoa kwenye makubaliano ya nyuklia na kuagiza kuuawa kwa jenerali aliyekuwa na mamlaka na nguvu kubwa nchini humo Qasem Soleimani.
Joe Biden anasema sera hiyo imefeli.
The post China, Urusi na Iran yaingilia uchaguzi wa Rais Marekani -Shirika la Ujasusi appeared first on Bongo5.com.