Mwanamke mmoja nchini Uingereza ameanguka kutoka ndani ya gari lake akiwa katika barabara kuu ya kwenda Westharm, baada ya mlango aliyokuwa akiutegemea kuchukua video ya Snapchat kufunguka ghafla.

Mwanamke huyo hakujeruhiwa vibaya lakini polisi wanasema “aliponea kifo”.

Alitibiwa katika eneo la tukio na wahudumu wa afya. Hakuna mtu aliyekamatwa, polisi walisema.

Katika ujumbe uliowekwa kwenye Twitter, polisi wakitengo cha usalama bara barani walisema: “Kiti cha abiria upande wa mbele kilikuwa kikining’inia nje ya gari wakati mwanamke huyo alipokuwa akichukua video ya Snapchat katika barabara ya M25. Baadae alianguka barabarani kutoka katika gari hilo. “Ana bahati sana hakujeruhiwa vibaya au kufariki. #sinalakusema”

Msemaji wa polisi katika eneo hilo alisema: “Maafisa waliitwa katika barabara kuu ya M25 mapema asubuhi kufuatia ripoti kwamba abiria ameanguka kutoka kwa gari lililokuwa likienda.

 

The post Anusurika kifo kisa Video ya Snapchat  appeared first on Bongo5.com.