Gazeti la mtandaoni la KINEDA limeripoti habari yenye msisimko wa kipekee, ambapo mwanaume mmoja aitwaye Jian Feng, amemshitaki mkewe kwa kumzaliwa watoto wenye sura mbaya. Bwana Feng anasema alimuoa mkewe kwa furaha na upendo, lakini furaha hiyo imetoweka na kuwasababishia mfarakano wa kindoa baada ya mkewe huyo kumzalia watoto wenye sura mbaya kiasi hata cha kuwaogopa.
Kwa bahati, baadaye mke wa Feng, alikuja kukikiri wazi na kuthibitisha kwamba, huko nyuma kabla hawajafunga ndoa, alipata kutumia kiasi cha dola $100,000 (€77,000) kufanyiwa upasuaji nchini Korea Kusini wa kujibadili mwonekano wake (Cosmetic surgery).
Kufuatia kukiri huko, Feng alimshitaki mkewe kwa kosa la kugushi mwonekano, na kutosema kweli juu ya upasuaji aliofanya kiasi cha kupelekea aonekane mrembo kinyume na uhalisia. Jaji alikubaliana na malalamiko ya Feng, na kumtakama mke alipe fidia ya dola $120,000 (€102900).