Chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania kinatarajiwa kuzindua rasmi kampeni zake hii leo kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28.

ACT itazindua kampeni mkoni Lindi kusini mwa Tanzania ambapo ndipo nyumbani kwa mgombea wake wa tiketi ya urais, bwana Benard Membe.

Wakati chama hicho kikizindua kampeni yake leo, vyama vingine viwili vikubwa karika uchaguzi huo Chadema na CCM tayari vinaendelea na kampeni.

Chama cha Chadema, ambacho ndicho chama kikuu cha upinzani kilizindua kampeni jijin Dar es Salaam Ijuu ilopita huku chama tawala CCM kikizindua kampeni Jumamosi.

ACT jana ilizindua ilani ya uchaguzi hapo jana ambayo wagombea wake watainadi katika kuomba kura ikiwa na vipaumbele 12 ikiwemo kutoa ajira mpya milioni 10 na ujenzi wa demokrasia na utoaji wa haki za watu.