Mapema leo Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini,CP Liberatus Sabas(kushoto) amewasili mkoani Morogoro kwaajili ya ukaguzi wa utayari kwa Askari mkoani humo katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani,(kulia) Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafugwa (PICHA NA JESHI LA POLISI)
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini, CP Liberatus Sabas akikagua Paredi la kutuliza ghasia (riot drill )paredi hilo limeundwa na askari  Polisi kutoka Mkoa wa Morogoro wakati wa mazoezi ya utayari kwaajili ya kukabiliana na uhalifu. (PICHA NA JESHI LA POLISI)
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini, CP Liberatus Sabas akizungumza na Maofisa na Askari Polisi wa vyeo mbalimbali  mkoani Morogoro baada ya kukakugua mazoezi ya utayari yaliyofanywa na askari wa mkoani humo.CP Sabas amewataka  Maofisa na askari hao kufanya kazi kwa bidii na kwa weredi kwa lengo la kuhakikisha nchi inaendelea kuwa kisiwa cha amani. (PICHA NA JESHI LA POLISI)