LEO tutangalia  madhara ya kula nyama… lakini kabla ya kuangalia madhara,  kuna makundi makuu mawili ya nyama yaani nyama  nyekundu na nyama nyeupe.


Nyama nyekundu ni ile ambayo ina rangi nyekundu kabla ya kupikwa,  mfano ya nguruwe, ng’ombe, mbuzi na wanyama wote wanaotembea kwa miguu minne.  Nyama nyeupe ni zile ambazo zina rangi nyeupe kabla ya kupikwa mfano kuku, bata, samaki, mbuni na wanyama wote wanaotembea kwa miguu miwili.

Utafiti unaonyesha ulaji wa nyama nyekundu una madhara makubwa  kuliko ulaji wa nyama nyeupe, hata hivyo, watu ambao hawali nyama kabisa wako mbali  na hatari hizi. Lakini kwa kuwa nyama pia ina faida katika miili yetu, basi nyama nyeupe ni salama  zaidi kuliko nyekundu.   Hebu tuangalie madhara ya nyama


1.Hatari ya kupata magonjwa ya moyo

Nyama ina kitu kinachoitwa lehemu, kitaalamu ni ‘cholesterol’.   Hii hukaa kwenye mishipa ya damu ya binadamu na kusababisha damu kushindwa kupita vizuri.. Hii husababisha viungo muhimu vya mwili kama moyo kukosa damu ya kutosha na kuanza kushindwa kufanya kazi. Japokuwa cholesterol ni muhimu kwenye mwili wa binadamu lakini inayotengenezwa na mwili inatosha.  Inayoongezeka kutoka kwnye nyama ni hatari sana.  (nyama nyekundu ina cholestrol nyingi zaidi)2. Kansa ya utumbo mkubwa

Nyama nyekundu ikiliwa inakaa masaa ishirini kwenye mfumo wa chakula wa binadamu tofauti na vyakula vingine. Utafiti unaonyesha limbikizo hilo linaambatana sana na hatari ya kupata ugonjwa wa kansa ya utumbo mkubwa. Lakini madhara ya haya yameonekana kutokuwepo kwa kula nyama nyeupe.3. Ugonjwa wa kisukari

Utafiti mpya umeonyesha kwamba watu wanaokula nyama na wasiokula nyama baada ya kufuatiliwa kwa muda wa miaka kumi mfululizo (cohort studies)… watu wanaokula nyama wameonekana kupata ugonjwa wa kisukari sana  kuliko wale wasiokula.


4. Hatari ya kupata ugonjwa wa Alzheirs disease

Huu ni ugonjwa wa akili ambao huwapata watu wengi uzeeni na dalili yake ikiwa ni kupoteza kumbukumbu kabisa. Wanasayansi wanaamini protini inayopatikana kwenye nyama kwa jina la Tau and beta-amyloid huharibu mishipa ya fahamu ya kwenye ubongo na kuchangia ugonjwa huu.5. Ugonjwa wa kifafa

Minyoo inyopatikana kwenye nguruwe kitaalamu kama ‘taenia solium’ hupanda mpaka kwenye ubongo na kuharibu mishipa ya fahamu ya ubongo hali ambayo husababisha kifafa kwa watu ambao hawakuzaliwa nacho kabisa. Hali hii inaweza kuzuiwa kwa kupika nyama hiyo kwa muda mrefu sana mpaka iive.6.Unene uliopitiliza

Nyama nyekundu ina kiwango kikubwa cha mafuta ambacho watu wengi hula mafuta hayo kama yalivyo, mfano kwenye nyama ya nguruwe.  Unene  na kitambi ni hatari sana kwani husababisha matatizo mengi ya kiafya na kisaikolojia, vifo vya ghafla vikiwa hatari zaidi kwenye suala la unene.7. Nyama tunazokula siku hizi si nyama halisi tena

Ukiangalia nyama ya kuku inayoliwa sana kwenye miji mikubwa na mahoteli, makubwa hapa nchini kwa kuku wa kisasa, utaona kuwa kuku hao wanakuzwa kwa kemikali nyingi  ambazo ni hatari kwa mwili wa binadamu na hata ladha yake ni tofauti kabisa na kuku wa kienyeji. Lakini kwa sababu wamiliki wa biashara za nyama ni watu wenye fedha nyingi, duniani ukweli huu hufichwa.8. Magonjwa ya wanyama husika

Miaka ya sasa dunia imekuwa inakumbwa na magonjwa ambayo mengi ni ya hatari. Na kama wewe tayari una tazizo la moyo, presha, kisukari na kansa, huu ni wakati sahihi wa kuacha kula nyama nyekundu kabisa kwani hizo nyama zitakupeleka kaburini.