Meneja na mfanyabiashara Petitman Wakuache amesema amewapatanisha Wema Sepetu na rafiki yake wa muda mrefu Aunty Ezekiel baada ya kuwepo na taarifa kwamba wawili hao  wanatofauti na imepita muda mrefu bila kuonekana wakiwa pamoja. 


Akitumia ukurasa wake wa Instagram kufikisha ujumbe huo Petitman Wakuache amepost video fupi akiwa na Wema Sepetu na Aunty Ezekiel huku akiwapa onyo kwamba ole wao wagombane tena. 

"Kama kawaida nipo na ndugu zangu wa ukweli kabisa, kwani mlipotelea wapi nishawapatanisha sasa ole wenu mgombane tena, kwa nini mliniacha mwenyewe sasa kwenye group mkaleft" amesema Petitman Wakuache