STAA kiwango wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu, ameweka wazi na kuvunja minong’ono kwamba, huwenda yeye ndiye mtarajiwa wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kama inavyoenezwa kwenye mitandao ya kijamii.

Tetesi hizo zimeibuka siku chache baada ya Diamond au Mondi kutangaza kuwa, yupo tayari kufunga ndoa ifi kapo Oktoba 2, mwaka huu, hivyo kuacha kitendawili cha nani atakayeolewa na Mondi.

Katika mahojiano maalum na gazeti hili la IJUMAA WIKIENDA, Wema amesema kuwa, yeye na Mondi ni watu waliobaki kuwa marafi ki tu wa karibu na hakuna kingine kinachoendelea kati yao kwa sababu kila mmoja ana uhusiano wake mwingine wa kimapenzi.

“Kuna wakati ninashangaa sana wanavyosema kuwa mimi ndiye mtarajiwa, inashangaza sana. Yule (Mondi) ni mshikaji wangu tu na si vinginevyo, wala watu wasiichukulie kihivyo. Nina mtu wangu jamani, anayeolewa na Nasibu (Mondi) siyo mimi,” amesema Wema ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Mondi kwa vipindi viwili kabla ya kumwagana jumla.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR