NDOA sasa inanukia! Kama ulikuwa hujui, taarifa ikufi kie kwamba, bidada Wema Isaac Sepetu yupo kwenye uchumba ‘siriaz’, lakini mwenyewe amesema hataki zile mahari kubwakubwa wanazojishaua nazo baadhi ya mastaa za shilingi milioni mia tano.

Wema ambaye ni mwigizaji wa Bongo Movies mwenye jina kubwa Afrika Mashariki, amekiri kuwa kwenye uhusiano huo wa kimapenzi na mwanaume ambaye jina na sura yake vimewekwa kwenye mabano hadi atakapomalizana na familia ya mrembo huyo juu ya suala hilo la mahari.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA juu ya taarifa za yeye kuolewa hivi karibuni na kwamba kuna maandalizi ya chinichini yanaendelea, Wema ameahidi kumuanika mwanaume huyo muda wowote akishakamilisha vitu fulanifulani vya nyumbani kwao.

Wema amesema anajua fi ka kwamba, watu wengi wanatamani kumjua mwanaume wake, lakini amewaomba kuvuta subira, kwani watamuona ‘soon’.

“Ni kweli kabisa hata mimi natamani kumuanika au kumposti kwenye ukurasa wangu (Instagram), lakini kuna vitu vikikaa sawa nitawaonesha, ila itakuwa baada ya kumaliza ishu za mahari,” amesema Wema ambaye ameshikilia Taji la Miss Tanzania mwaka 2006/07.

Wema amesema ana uzoefu mkubwa katika mahusiano yake yaliyopita, hivyo anafahamu umuhimu wa kumfi cha au kutomuanika mtu wake kabla ya kukamilisha taratibu fulanifulani. Kuhusu mahari, Wema anasema hawezi kusema anahitaji mahari kubwa za mamilioni hadi milioni mia tano, bali anachohitaji ni makubaliano tu ya huyo mtu wake na familia yake.

“Hapana, mimi siwezi kusema nataka milioni mia tano, vyovyote atakavyokubaliana na familia yangu ndivyo hivyo,” anasema Wema ambaye uchunguzi wa gazeti hili umebaini, kwa sasa ana furaha mno baada ya kumpata mwanaume huyo.

Mara ya mwisho Wema kusemekana anaolewa, ni kipindi kile cha jamaa aliyejiita PCK ambaye baadaye alipata msala wa utapeli na mikakati ya ndoa ikaishia hapo ambapo Wema amekuwa msiri mno wa kumuonesha mpenzi wake.

Wema kwa sasa ana umri wa miaka 31, hivyo ni wakati muafaka kwake kuingia kwenye ndoa na kupata mtoto, kwani amekuwa na shauku ya kupata mtoto kwa muda mrefu.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR