Ratiba ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara imetoka rasmi hii leo siku ya Jumatatu ya tarehe 17/08/2020. Katika ratiba hiyo Mabingwa watetezi Simba watakuwa ugenini kwenye mchezo wao wa kwanza kuwakabili wageni wa ligi kuu IHEFU FC Uwanja wa Sokoine tarehe 6/ 9/ 2020 saa 10: 00 Alasiri.

Kariakoo Derby: Morrison the hero as Yanga SC down Simba SC | Goal.com

Mabingwa wa kihistoria Yanga wao mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu watakuwa nyumbani dimba la Mkapa wakiwaalika Tanzania Prisons siku hiyo hiyo ambayo watani wao wakiwa wanashuka uwanjani.

Mchezo wa Watani wa Jadi kwa mujibu wa ratiba hii utapigwa siku ya Jumapili Oktoba 18, 2020 majira ya saa 11:00 jioni wakati Young Africans Sports Club wakiwa wenyeji ambapo watawakaribisha Mabingwa wa Nchi Simba Sports Club.

RATIBA KAMILI -> Ratiba VPL 20202021_20200817113109

The post Watani wa jadi kukutana Oktoba, ifahamu timu mwenyeji appeared first on Bongo5.com.