Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Simba ambaye ni mwekezaji wa timu hiyo, Mohammed Dewji amewataka Wanachama, Mashabiki na wapenzi wa soka kutulia na kuwakumbusha kuwa wametoka mbali na wameyapitia mengi.

Mo ameandika ujumbe huo muda mchache tu baada ya Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Senzo Mazingisa kutangaza kujiuzulu na kuwepo na tetesi kuhamia upande wa pili kwa hasimu wao Yanga SC.

‘Tumetoka mbali na bado safari inaendelea; tumepita mengi Wanasimba wenzangu. Nawaomba Wanasimba wote mtulie. SIMBA SC ni kubwa kuliko mtu moja. Sisi viongozi tunawatumikia usiku na mchana bila kujali maslahi ya mtu binafsi bali SIMBA. Kazi inaendelea, tuko IMARA!,” – Mo Dewji

 

IMEANDIKWA NA HAMZA FUMO, Instagram @fumo255

The post Wanasimba mtulie, Simba ni kubwa kuliko mtu mmoja, tuko Imara – Mo Dewji appeared first on Bongo5.com.