Wahusika wa mapinduzi ya Mali yaliomuondoa rais wa taifa hilo Ibrahim Keita siku ya Jumanne ni pamoja na naibu kiongozi wa kambi za kijeshi na jenerali aliepata mafunzo yake nchini Ufaransa.
BBC Monitoring imewaangazia viongozi watatu wanaodaiwa kuchukua majukumu muhimu katika mapinduzi hayo.
1. Kanali Malick Diaw
Ni naibu kiongozi wa kambi ya jeshi ya kati ambapo mapinduzi hayo yalianzia.
Kuna habari chache kumuhusu mbali na ripoti kwamba alitoka katika mafunzo ya kijeshi nchini Urusi.
Alisimama kandakando ya naibu afisa mkuu wa jeshi kanali Ismale Wague ambaye alisoma taarifa siku ya Jumatano kwa niaba ya vuguvugu la Junta ili kutangaza mapinduzi hayo ya kijeshi.
Kanali Diaw anaaminika kuwa kiongozi wa mapinduzi katika kambi hiyo ya Kati , kilomita 15 kutoka Bamakoi.
Anadaiwa kumuomba rais kuondoka madarakani kabla ya saa nane mchana, ujumbe wa twitter ulisema kumuhusu.
2. Kanali Sadio Camara
Kanali Camara ni mkurugenzi wa zamani wa chuo cha mafunzo ya kijeshi.
Tovuti ya Mali iliripoti kwamba alizaliwa 1979 katika eneo la Kati, katika jimbo la Kusini la Koulikoro. Alifuzu kutoka chuo cha kijeshi cha Koulikoro .
Baadaye alipelekwa katika eneo la kaskazini mwa Mali ambapo alihudumu chini ya jenerali El Hadj Gamou hadi 2012.
Kanali Camara baadaye alikuwa mkurugenzi wa chuo cha mafunzo ya kijeshi cha Kati , nafasi alioshikilia hadi Januari 2020 wakati alipoelekea Urusi kwa mafunzo ya kijeshi.
Gazeti la Mali Tribune lilisema kwamba alirudi Bamako mapema mwezi huu ili kuchukua likizo yake ya mwezi mmoja.
Kanali Camara alipendwa na kila mtu ambapo alifanya kazi na anaheshimiwa na wadogo zake wote.
Kwa wao , anawakilisha haki, mtu mwenye umakini, na mwenye ari ya kufanya kazi, ilisema tovuti hiyo.
3. Jenerali Cheick Fanta Mady Dembele
Jenerali Cheick Fanta Mady Dembele ni mkurugenzi wa taasisi ya kuweka amani ya Alioune Blondin Beye .
Alipandishwa cheo hadi kufikia cheo cha Brigedia jenerali na kuchukua uongozi wa taasisi hiyo ya kulinda amani mwezi Disemba 2018..
Kabla ya kupandishwa cheo katika taasisi hiyo , jenerali Dembele alikuwa akisimamia migogoro na mipango ya kimkakati katika tume ya amani na usalama barani Afrika ilio na makao yake makuu Addis Ababa, Ethiopia.
Jenerali Dembele alifuzu katika chuo kikuu cha kijeshi cha Saint-Cyr military nchini Ufaransa .
Pia alihitimu kutoka chuo cha General Staff College huko Koulikoro, Mali.
Anamiliki shahada katika historia kutoka chuo kikuu cha Paris cha I Panthéon-Sorbonne.
Pia anamiliki stashahada katika uhandisi na alifuzu kutoka chuo kikuu cha Federal Army University mjini Munich, Ujerumani.
The post Wafahamu viongozi watatu wa juu wa kijeshi waliipindua Serikali ya taifa la Mali appeared first on Bongo5.com.