Dodoma, Tanzania

WanaCCM waandamana kupinga maamuzi


Vurugu zinaendelea leo 18 agosti 2020 katika ofisi za CCM Wilaya ya Dodoma mjini baada ya kupokea majina ya wagombea udiwani ambao wamekatwa licha ya kuongoza.

Jana halmashauri ya CCM mkoa wa Dodoma walirudisha majina ya madiwani waliogombea kupitia chama hicho ambapo kata 7 Kati ya 41 za jiji la Dodoma walioongoza walikatwa na kurudishwa wengine ndipo wakaandamana ofisi za wilaya.

Mmoja wa diwani aliyeshinda CCM lakini jina lake lililokatwa amewaomba wanaCCM wa kata ya Changombe kuwa watulivu wasifanye maandamano wasubiri maamuzi ya Halmshauri ya wilaya CCM watakapotafuta ufumbuzi wa sintofahamu hiyo ndani ya CCM .

Chanzo: Mwananchi digital



#CloudsDigitalUpdates

Vurugu zimeibuka katika ofisi za Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Dodoma baada ya Makada wa CCM wanaodai Majina ya Wagombea Udiwani yaliyopitishwa yamebadilishwa bila Sababu za Msingi katika baadhi ya kata za Wilaya ya hiyo kuweka kambi katika ofisi hizo.

MINUDI DANIEL ni katibu wa CCM kata ya Ipagala amejikuta katika wakati Mgumu baada ya kutoka katika ofisi za chama hicho ili kuwaeleza wanachama wake kinachoendelea baada ya kudai kupokea agizo la kutakiwa kurudisha barua aliyokwishapewa ili kumpatia mgombea aliyepitishwa kugombea kata hiyo kwaajili ya marekebisho.