Wizara ya mambo ya kigeni ya Ufaransa imetoa onyo kali kwa raia wake dhidi ya kusafiri kwenda Niger, baada ya raia sita wa taifa hilo kuwa miongoni mwa watu wanane waliouawa na washukiwa wa itikadi kali mwishoni mwa wiki.

Tovuti ya wizara hiyo imesema watu wanatahadharishwa kutosafiri nchini humo, ukiachilia mbali mjini mkuu Niamey, ambao pia wameshauriwa kutokwenda isipokuwa tu kwa sababu za lazima.

Ushauri huo mpya unamaanisha kwamba sehemu ya kaskazini mwa Niger, ambayo ni karibu robo ya taifa hilo, imejumlishwa kwenye kile kinachoitwa ukanda wa hatari, ambao unapendekezwa kuepukwa.
Taifa hilo maskini liko katikati mwa kanda ya Sahel, ambayo imevurugwa vibaya na uasi ulioanzia kaskazini-mashariki mwa Nigeria mwaka 2010 na nchini Mali mwaka 2012.
The post Ufaransa yawaonya raia wake kwenda Nigeria appeared first on Bongo5.com.