Mbivu na Mbichi kujulikana wakati vinara wa soka Ulayawatakapokabana koo!

Kiu ya mashabiki wa soka ulimwenguni waliyokuwa nayo baadaya kuahirishwa kwa mashindano ya UEFA sasa itapoa baada yakutangazwa kurejea kwa michuano hiyo. Wateja wa SuperSportkupitia DStv sasa wakae mkao wa kula kwani kuanzia Agosti 7 wataanza kushuhudia vinara wa soka Ulawa yakikabana kookuwania ubingwa huo. Zitakuwa ni wiki mbili za moto mkaliambapo michezo 11 inayozihusisha timu kubwa za sokaulimwenguni itanguruma.

 

Wakati patashika hii ikirejea tena, wababe kama vile RB Leipzig, Atletico Madrid, Paris Saint-Germain na Atalanta – wote wananafasi kubwa ya kuutwaa ubingwa kwani wanahitaji kushindamichezo mitatu tu japo wote wako pamoja hivyo ni mmoja tuataingia fainali!

 

 

Wakati washiriki kutoka nchi nyingine wakiwa na wakati mgumukutokana na ama ligi zao kufutwa au kuwahi kuisha, washirikikutoka Uingereza– Chelsea na Manchester City wanakuja na moto mkali kwani ligi yao ilikamilika muda simrefu uliopita hivyo badowana mzuka, japo pia wanaweza kuwa wameathiriwa na uchovu

 

Wenye ahueni kubwa ni vinara wa Hispania – Atletico Madrid, Real Madrid na Barcelona ambao walipata wiki kadhaa za kupumzika baada ya kukamilika kwa La Liga.

 

Patashika itaanza Ijumaa hii wakatiJuventus watakapomenyana naLyon huku Manchester City ikiumana na Real Madrid. Jumamosiwababe Bayern Munich watakipiga na Chelsea huku Barcelona wakitoana jasho na Napoli. Fainali ya michuano hii itafanyikaJumapili 23 Agosti 2020

 

Wateja wa DStv wataweza kushuhudia michuano hiyo mubasharana kwa kutumia huduma ya DStv Now, mteja anaweza kufuatiliamichuano hii popote alipo kwa kutumia simu yake au kompyutabila malipo yoyote ya ziada kwenye kifurushi husika.

The post UEFA Champions League Mubashara ndaniya DStv! appeared first on Bongo5.com.