Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema hakuna madhara yaliyotokea kupitia tetemeko la ardhi lilitokoa jana usiku katika maeneo mbalimbali Tanzania.

“Kutokana na kutokea kwa Tetemeko la Ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha 5.9, chini ya Bahari, TMA imefanya uchambuzi wa taarifa za Tetemeko hilo na hakuna tishio la Tsunami kutokana na Tetemeko hilo kwakuwa alikua na nguvu kubwa na hakuna maporomoko yaliyojitokeza Baharini”-Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)

“Hakuna athari zilizojitokeza au zinazotarajiwa katika mifumo ya hali ya hewa ya Bahari kutokana na Tetemeko la jana usiku, TMA inawashauri watumiaji eneo la Bahari wakiwemo Wananchi wanaoishi maeneo yaliyo karibu na Bahari ya Hindi kutokuwa na hofu na kuendelea na shughuli”-TMA

The post TMA: Hakuna madhara ya tetemeko yaliojitokeza, wananchi waendelee kuchapa kazi appeared first on Bongo5.com.