Mwanasiasa mkongwe na mmoja wa waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Hassan Nassor Moyo amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mkoani Tanga.

Mzee Moyo ambaye aliwahi kuwa Waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar, amefikwa na mauti hayo baada ya kusumbulia na maradhi kwa muda mrefu. Taratibu za msiba huo zinaendelea huko Tanga.

Inna lillah wainna ilayhi rajiuna.