Je wewe ni mpenzi wa muziki wa hip-hop na una fedha zinazokuwasha mifukoni mwako? basi huenda huu ni wakati wako. Vazi lenye historia katika muziki wa hip-hop linapigwa mnada – taji hilo la kifalme lilivaliwa na msanii nyota Notorious B.I.G. wakati alipokuwa akipiga picha za nyimbo zake za mwisho.
Picha hiyo kwa jina Mfalme wa New York , kama ilivyojulikana imechapishwa katika majarida tofauti , kanda za muziki , tisheti, katika kuta na hata katika msururu wa filamu ya NetFlix kwa jina Luke Cage.
Ni miongoni mwa vitu vinavyopigwa mnada katika jumba la Sotheby, mchango wa muziki wa hip-hop ambao unashirikisha barua za mapenzi zilizoandikwa na Tupac Shakur akiwa na umri wa miaka 16.
Baadhi ya fedha ziliuzokusanywa kupitia vitu 120 vinavypigwa mnada zitatumika katika miradi ya kijamii mjini New York.
Taji la kifalme lililovaliwa na kutiwa saini na Biggie
Biggie alivalia taji hilo siku tatu kabla ya kupigwa risasi hadi kufa mnamo tarehe 9 mwezi Machi 1997. Msani hyo wa muziki wa rap na mpiga picha wake Barron Claiborne waliitia saini wakati huo na Barron amekuwa akilimiliki tangu wakati huo.
”Nafurahi sana kugawana taji hili la kihistoria na umma”, anasema.
Kifa hicho kilibadili umaarufu wa Biggie Small kuwa kama ule wa mtakatifu na mtu wa tabaka la juu katika jamii, na kuchukuliwa sio tu kama mfalme wa New York , lakini pia mfalme wa muziki wa Hip Hop na msanii mkubwa wa kizazi chake.
Jumba la mnada la Sotheby linataraji kwamba taji hilo la kifalme litakusanya kati ya $200,000 hadi $300,000 .
Taji hilo linapendwa sana wakati huu ijapokuwa msimamizi wa nembo ya Biggie ambaye alikuwa naye wakati wa shambulio hilo , aliripotiwa kuwa na wasiwasi wakati huo ilipoonekana kufanana na mfalme wa Burger badala ya yule wa muziki wa hip-hop.
Barua za mapenzi za Tupac Shakur
Kuna barua 22 za mapenzi zilizotiwa saini na Tupac Shakur akiwa na umri wa miaka 16 na kutumwa kwa Kathy Loy wakati walipokuwa wapenzi katika shule ya sanaa ya Baltimore 1980.
Tupac Shakur alituma barua hizo wakati walipokuwa na uhusiano wa miezi miwili na angemalizia kwa njia tofauti. “Mpenzi, Tupac”, “Milele, Tupac”, “Mapenzi tele, Tupac”, “Mimi wako wa Maisha, Tupac” na “Na Moyo Wangu, Tupac”.
Barua hizo zinazungumzia kuhusu mkutano wao wa kwanza hadi penzi lao lilipovunjika, na barua ya kujuta iliotumwa mwaka mmoja baadaye. Zote zinakadiriwa kuwa na thamani $60,000 hadi $80,000
The post Taji la kifalme la msanii Notorious B.I.G. na barua za mapenzi za Tupac Shakur kuuzwa katika mnada appeared first on Bongo5.com.