Salamu za rambi rambi kwa watu wa Lebanon zimetumwa kutoka sehemu mbalimbali Duniani, ikiwemo jirani zake Israel ambao walisema haraka kwamba hawajahusika na mlipuko huo.

Lebanon's president says ammonium nitrate caused blast

Rais wa Lebanon, Michel Aoun ametoa wito kwa Baraza la Mawaziri kutangaza wiki mbili za hali ya dharura ya kitaifa huko Beirut baada ya mlipuko mkubwa mapema Jumanne ulioharibu sehemu kubwa ya bandari ya mji huo na kuuwa watu 78 na kuwajeruhi zaidi ya 3,500.

Japokuwa chanzo rasmi cha mlipuko huo hakijulikani, Aoun aliandika kwenye mtandao kwamba ”Sitapumzika hadi tunampata mtu aliyehusika na kile kilichotokea na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria na kumhukumu”.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Lebanon, Hassan Diab alikutana na wizara ya ulinzi Jumanne usiku kwa saa za huko akielezea uungaji mkono wake kwa watu anaowaita “mashahidi” na kuwatakia majeruhi nafuu ya kupona haraka.

Pia alitaka kamati ya uchunguzi iundwe haraka. Diab ametangaza Jumatano ni siku ya maombolezi nchini Lebanon.

Rais wa Marekani Donald Trump alisema Jumanne wakati akitoa maelezo mafupi kuhusiana na janga la virusi vya Corona huko White House, kwamba “Marekani ipo tayari kuisaidia Lebanon. Tutakuwepo nao kuwapa msaada. Inaonekana ni shambulizi baya sana”

Source Voice of America

The post Sitapumzika mpaka nampata aliyehusika na mlipuko – Rais wa Lebanon aapa appeared first on Bongo5.com.