Na: Faustine Gimu
Waziri  wa Mambo yaNdani George Simbachawene amevitaka vyombo vya usalama nchini kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya Usafirishaji   wa  binadamu  ambayo  imekuwa  ikifanyika ndani ya nchi na nje ya  nchi.

Waziri Simbachawene  ameyasema  hayo    jijini Dodoma katika  maadhimisho  ya siku  ya  kupinga   biashara   haramu   ya   usafirishaji   wa   binadamu yaliyohusisha   wadau   mbalimbali   ambapo biashara   hiyo    hufanyika    mataifa   mbalimbali        duniani.

Amebainisha  kuwa Wizara   itajikita   kusimamia   safari za  ndani ya  nchi kwa lengo la kubaini wanaojihusisha na vitendo hivyo  ambapo amebainisha kuwa waathirika  wakubwa  ni wanawake na watoto vitendo ambavyop hutokana sababu mbalimbali ikiwemo  tama  ya  pesa  na kuibuka  kwa  soko la vitendovya ngono.

Akizungumzia watanzania  wanaotaka kufanya kazi nje ya  nchi  amewata  kufuata sheria na taratibu zilizowekwa  badala ya   kuzamia kwa   kutumia njia haramu kwa  kigezo cha    kutafuta maisha  akisisitiza kujiridhisha  kuhusu kazi husika kabla  ya  kufanya  maamuzi  ya   kwenda   nje ya nchi.

Mwenyekiti wa Kamati ya  Taifa ya Kuzuia  na  Kupamba  na  biashara  haramu  ya usafirishaji wabinadamu  Amatus Magere katika amesema mapambano  hayo wanakabiliwa na changamoto nyingi kwani hufanywa na binadamu wenyewe kwa siri kubwa ,kukosekana kwa mfuko wa  kusaidia waathirika na upungufu wa raslimali watu