Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, akimwangalia mtoto wa Kirundi alipokuwa anacheza ngoma ya asili ya nchini Burundi, kabla ya Waziri huyo hajazungumza na Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, Wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma, leo.  Simbachawene amefuta  utaratibu uliokua umewekwa kwa wakimbizi nchini pindi wanapokamatwa kutopelekwa mahakamani badala yake warudishwe nchini kwao, hivyo kuanzia sasa mkimbizi yeyote atakayekutwa na makosa atapelekwa mahakamani kisha jela endapo atakutwa na makosa ya kihalifu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, akizungumza na Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, Wilayani Kasulu, Mkoani Kigoma, leo, ambao wanasubiri kupanda mabasi kurudishwa nchini kwao kwa hiari. Amewapongeza Wakimbizi hao kwa kufanya maamuzi ya busara kurudi nchini kwao kwasababu sasa nchi hiyo inja amani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Sudi Mwakibasi, alipokuwa anazungumza na Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, Wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma, leo.  Simbachawene amefuta  utaratibu uliokua umewekwa kwa wakimbizi nchini pindi wanapokamatwa kutopelekwa mahakamani badala yake warudishwe nchini kwao, hivyo kuanzia sasa mkimbizi yeyote atakayekutwa na makosa atapelekwa mahakamani kisha jela endapo atakutwa na makosa ya kihalifu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.