BAADA ya uongozi wa Yanga kusema kuwa unashangazwa na shinikizo kutoka kwa Wizara ya Uhamiaji kuitaka timu hiyo kutoa kibali cha kazi kwa nyota wao wa zamani, Bernard Morrison, Simba nao wamewajibu kimtindo watani zao wa jadi.

Morrison alikuwa kwenye mvutano mkubwa na mabosi zake Yanga kwenye ishu ya mkataba ambapo yeye alikuwa anadai kwamba ana dili la mwaka mmoja huku Yanga wakieleza kuwa ana dili la miaka miwili.


Shauri hilo lilisikilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 10 mpaka Agosti 12 ambapo majibu yalipotolewa makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) yalieleza kuwa Morrison ni mchezaji huru na ameshinda kesi yake hiyo.


Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa:"Naishangaa Wizara ya Uhamiaji inaposhinikiza tutoe kibali cha Morrison, inaonesha kama kuna 'Interest'. Kama kutolewa kinatolewa lakini kwa taratibu maalumu."


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amejibu namna hii:"Nimeskia mmoja kaanza kuilaumu Wizara ya Uhamiaji , sikujua kuwa Bongo kuna hii wizara."