Mtandao wa kandanda.co.tz umekabidhi tunzo ya Galacha Oyee katika kipengele cha ‘Timu Galacha ya Msimu‘ kwenda kwa klabu ya Simba SC ya jijini Dar es salaam, ikiwa ni Tunzo ya kwanza kwa klabu baada ya utaratibu wa kusheherekea na timu pamoja na wachezaji wanaofanya vizuri katika msimu unaomalizika.
 
Tunzo hii imekabidhiwa kwa niaba ya mtandao huo na Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Bima ya MGen, Jackson Kindikwili na kupokelewa na Mratibu wa Shughuli za Simba, Abbas Ally ambaye alishukuru na kuupongeza mtandao huo kwa kutambua mchango wa klabu yao na kwa ubunifu wa tunzo hiyo. 
 
Ikumbukwe klabu hii ilitoa Galacha wa Mabao wa msimu uliopita, na alikabidhiwa zawadi yake mapeka baada ya mashindano. Pia mtandao huo umekuwa ukitoa zawadi kila mwezi kwa wachezaji wanaofunga mabao mengi kwa mwezi husika.
 
Klabu ya Simba ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa misimu mitatu mfululizo sasa, wakifanya vizuri katika kuongoza Ligi na Ufungaji wa mabao pia.
 
Simba ilipata pia matokeo mazuri katika msimu wa 2019/20 dhidi ya vilabu vitatu Yanga, Azam na Tanzania Prisons ambavyo kwa msimu mitatu timu hizi zimeshika nafasi nne za juu.
Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Bima ya MGen, Jackson Kindikwili  (katikati) akikabidhi Tunzo hiyo kwa viongozi wa Timu ya Simba ambao ni wa pamoja na Abbas Ally (Kushoto) na Meneja wa timu ya Simba, Patrick Rweyemamu (Kulia).