Usiku wa Agosti 7, 2020 zilitolewa tuzo za Ligi Kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20 ambapo abingwa wa soka nchini Simba SC walitawala huku tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20 ikichukuliwa na Clatous Chama wa Simba. SC.

Tuzo ya Heshima imeenda kwa nguli wa soka wa zamani ambaye pia ni baba mzazi wa msemaji wa Simba SC Haji Manara, Mzee Sunday Manara.

Kiungo Bora wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20 ni Clatous Chama wa Simba SC.

Beki Bora wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20 ni Nicolaus Wadada wa Azam FC.

Mwamuzi Bora wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20 ni Ramadhan Kayoko.

Mwamuzi Bora msaidizi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara ni Frank Komba.

Tuzo ya Golikipa Bora wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20 imeenda kwa kipa wa mabingwa Aishi Manula.