Messi wa BongoFleva Rich Mavoko amefunguka kusema ilikuwa mipango na malengo yake kuwa kimya kwa muda mrefu, na comment aliyoiachia Harmonize kwenye mtandao wa Instagram kuhusu ukimya wake anaitafsiri kama ni hisia kwani aliishi naye vizuri. 


Rich Mavoko ameendelea kusema ilikuwa ni lazima kurudi nyuma na kupanga vitu sawa ndiyo maana aliamua hata asiwepo kwenye mitandao ya simu ili kuji-update na kuwa mpya. 


"Wakati Harmonize anaandika ile comment nilikuwa sina mawasiliano naye, pili niliichukulia kama alikuwa hajui nipo wapi na nafanya nini labda kwa sababu alihisi kuna vitu vinaongeleka, alikuwa na haki ya kuandika anachohisi kutokana hisia zake na aliyokuwa anayaona, pia yule ni mdogo wangu na niliishi naye vizuri" ameeleza Rich Mavoko