Wakuu kama kichwa kinavyooleza hapo ugomvi wa Komando huyu wa kike kwenye tasnia ya burudani ya Muziki wa Bongo Fleva umezikwa, leo tangu asubuhi bandika bandua ni ngoma tu za Lady Jay Dee zinapigwa kumpa promo kwenye tamasha lake la miaka 20 yake kwenye tasnia.

Hivi ndivyo inavyotakiwa Clouds iwape uwanja sawa wasanii wote bila kubagua tutafika mbali, sifahamu kama amelipia au bure lakini cha msingi promo kama hii ifanyike kwa wasanii wote na kwa vituo vyote itasaidia kukuza mziki.