Rapa maarufu wa Marekani, Mathew Matthers Eminem, amezushiwa kufariki dunia usiku wa kuamkia leo mara baada ya hashtag ya #RipEminem kusambaa kwenye mtandao wa Twitter.


Hashtag hiyo iliyoibua taharuki KUBWA kwa wapenzi wa msanii huyo (mashabiki) ikawalazimu kutafuta chanzo cha taarifa hiyo na baaadaye ilioneka tweet kutoka kwa jamaa mmoja iliyosomeka "I have Killed eminem"

-

Hata hivyo baadhi ya mashabiki waliaanza ku-share salamu zao za rambirambi wakidhani ni kweli #Eminem amefariki. Wengine wameitafsiri kama sio kifo cha kawaida bali ni kifo cha kimuziki.Aidha, hadi sasa bado Eminem na uongozi wake hawajasema chochote juu ya taarifa hiyo.