Mkutano wa 40 wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini ya Afrika (SADC) unatarajiwa kufanyika leo Chamwino mkoani Dodoma.

Katika mkutano huo Rais John Magufuli anatarajiwa kukabidhi jukumu la uenyekiti wa SADC kwa Rais wa Msumbiji Philipe Nyusi.

Mkutano wa Dodoma utafanyika kwa njia ya video kwa kuongozwa na Rais wa Msumbiji. Kaulimbiu ya mkutano huo ni;’Miaka 40 ya kuimarisha amani na usalama, kukuza maendeleo na kuhimili changamoto zinazoikabili dunia’

Rais Magufuli amekuwa Mwenyekiti SADC kwa mwaka mmoja. Alikabidhiwa jukumu hilo Agosti mwaka jana kutoka kwa Rais wa Namibia Dk Hage Geingob.