Rais wa zamani wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita amerejea nyumbani hapo jana baada ya kuwekwa kizuizini kwa siku 10 na jeshi linaloshika atamu ya uongozi, baada ya kufanya mapinduzi juma lililopita.
Taarifa hiyo ni kwa mujubu wa familia yake. Hatua hiyo inatekelezwa sambamba na tangazo la kijeshi la kuongoza taifa hilo katika kipindi cha mpito ikitazamwa kama hatua ya kwenda kinyume na katiba ya Mali.
Keita alikamatwa Agosti 18 na kundi la maafisa wa kijeshi na kumpeleka eneo la umbali wa kilometa 15 kutoka mjini Bamako, ambapo baadae alitangaza kujiuzulu urais.
Viongozi wa mataifa wa Jumuiya ya Maendeleo Afrika Magharibi ECOWAS, umoja wenye mataifa 15, wamepinga vikali kuondolewa madarakani kwa kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia na wameiwekea vikwazo Mali, kwa kufunga mipaka, vizuizi vya kibiashara na kutishia vingine zaidi.
The post Rais aliyepinduliwa najeshi Mali, arejeshwa nyumbani kwa ulinzi mkali appeared first on Bongo5.com.