Staa wa muziki nchini, Linah amesema yeye na mchezaji wa Simba SC, Bernard Morrison ni marafiki tu na sivyo kama inavyo zungumzwa.


Hapo jana ilisambaa picha mitandaoni, ikiwaonesha wawili hao wakiwa pamoja wakicheza game huku nyuso zao zikiwa na furaha, hali iliyopelekea kuwepo na maneno mengi juu yao.

“Mimi na Morrison ni washkaji tu, ninaweza kusema yeye ni shabiki yangu na mimi ni shabiki yake, tulikutana katika Mazingira fulani ambayo hata mimi sikutegemea kama ningekuwa hapo, alivyoniona alisema ni mwanamuziki anayenifuatilia kazi zangu kitambo,” ameeleza.
“Alivyoniita nikaingia hiyo sehemu aliyokuwepo alikuwa anacheza ‘game’ na washkaji zake tukapiga picha, sio mpenzi wangu,” ameeleza Linah.
Morrison ambaye hivi karibuni aligonga sana vichwa vya habari hapa nchini, kwa sasa ni mchezaji rasmi wa Simba SC mara baada ya kushinda shauri lake dhidi ya Yanga SC aliyokuwa akiichezea awali.