Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ndugu Andrew Masawe amezitaka OSHA na CMA kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha kunakuwepo na usalama na Afya katika maeneo ya kazi sambamba na kupunguza migogoro sehemu za kazi.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao kazi kati ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) pamoja na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) mkoani Morogoro,Bwana Masawe amesema OSHA na CMA zina mahusiano yanayotegemeana, na ili eneo la kazi liweze kuwa na usalama na afya nzuri kwa wafanyakazi na kusiwe nashida sehemu za kazi kunatakiwa haki itendeke, sheria, kanuni na miongozo iweze kufanyiwa kazi vizuri. Sehemu inapoonekana kuna migogoro ni vizuri CMA kwenda na kutenda haki sehemu ya kazi.

Masawe ameongeza kuwa sehemu ya kazi zinapokuwa hazina migogoro basi wafanyakazi wanafanya kazi kwa amani na hivyo uzalishaji unaongezeka. Aidha Bwana Masawe alisema Katika kipindi cha mwaka 2019/2020 CMA imeweza kusuluhisha Jumla ya zaidi Migogoro elfu 10 ambayo ni sawa na asimilia 81, Huku migogoro zaidi ya elfu 6 sawa na asilimia 77 ikitolewa uamuzi.

“Nitoe wito kwa CMA kuendelea kutoa elimu zaidi kwenye maeneo ya kazi, ili wafanyakazi wapate uelewa zaidi namna wanavyofanya kazi, kwasababu OSHA ipo maeneo mengi ya kazi, hivyo wanapokuwa huko basi CMA nanyi mkatoe elimu zaidi ili wafanyakazi waweze kujua namna mnavyofanya” alisema Masawe.

Naye kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi Khadija Mwenda amesema lengo la kikao kazi hicho ilikuwa, ni kujadiliana namna gani ya kutatua migogoro sehemu za kazi ili kupunguza migogoro isiyo ya lazima sehemu za kazi.

Amesema migogoro inapotokea ndio inaenda CMA. majadiliano hayo yamelenga kuhakikisha kuwa migogoro sehemu za kazi zinapungua , amesema kupitia kikao
kazi hicho, kuhakikisha.

Amesema migogoro inapokuwa mingi inarudisha nyuma lengo la serikali katika
kufikia uchumi wa viwanda, muda mwingi unatumika katika kutatua migogoro na kulipa fidia, panapokuwa na uelewa wa pamoja basi azma ya kufikia kujenga uchumi wa Viwanda kwenda mbele.

Mwenda amesema watu wengi wameajiriwa kwenye sekta za uzalishaji, na huko ndiko ampambo sheria sizipo angaliwa vizuri zitarudhisha nyuma juhudi za serikali kufikia malengo na hivyo kukwamisha uzalishaji.

Kwa upande wake Afisa Mfawidhi Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Ndugu Usekelege Nahshon Mpulla amesema mafunzo haya waliyoyapata yatakuwa msaada katika kazi zao, hivyo ni muhimu kwa waajiri na wafanyakazi kufahamu sheria ya OSHA na kufuata ili kuweza kuahikisha usalama na afya unakuwepo sehemu za kazi, ili kuweza kusaidia katika kukuza uchumi.

The post OSHA na CMA zatakiwa kushirikiana kuhakikisha Usalama na Afya unakuwepo mahala pa kazi (+Video) appeared first on Bongo5.com.