Staa wa muziki nchini, Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz ameweka wazi kuwa yupo mbioni kuachia Album.


Dimpoz ambaye ni mmoja kati ya wasanii wenye masihara na maneno mengi ya kuchekesha, hii itakuwa ni Album yake ya kwanza katika maisha yake ya muziki wa Bongo Fleva.


Kupitia ujumbe ambao ame-uambatanisha na post yake ya video kwenye ukurasa wake wa #Instagram, Dimpoz amedokeza ujio wa Album hiyo bila kutaja tarehe RASMI ya kuiachia.


Aidha, Ommy Dimpoz anaongezeka kwenye listi ya wasanii watakao achia Album zao mwaka huu, wasanii wengine ni pamoja na #LadyJaydee, #Weusi, #NavyKenzo, #Harmonize n.k