Ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini za Arusha mjini usiku wa kuamkia leo Agosti 14, 2020,  zimeteketea kwa moto na chanzo cha moto huo hakijajulikana.

Kwa mujibu wa Chadema, watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wamevamia na kuchoma moto ofisi za chama hicho Kanda ya Kaskazini  na ofisi za Mkoa na Wilaya

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, chama hicho kimeeleza kuwa kinaendelea kuangalia ili kubaini kama kuna hatari zaidi inayoweza kuwepo. Moto huo umezimwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limesema litatoa taarifa baada ya uchunguzi kukamilika kuhusu kuungua moto ofisi za CHADEMA Kanda ya Kaskazini.