Mwanamuzi nchini katika jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Kano amehukumiwa kifo kwa kunyongwa kwa kumkufuru Mtume Mohammad.

Mahakama ya juu ya kiislamu inayotumia Sharia katika eneo la Hausawa Filin Hockey katika jimbo la Kano imesema kuwa Yahaya Sharif-Aminu, mwenye umri wa miaka 22, alipatikana na hatia ya kukufuru kwa wimbo wake uliosambazwa kupitia mtandao wa WhatsApp mwezi Machi.

Bwana Sharif-Aminu hakukanusha mashitaka.

Jaji Khadi Aliyu Muhammad Kani alisema kuwa anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo dhidi yake.

Majimbo ya kaskazini mwa Nigeria yanayokaliwa na Waislamu wengi hutumia sheria ya kiislamu na sheria ya kawaida, ambayo haitumiwi kwa watu ambao sio wafuasi wa dini ya kiislamu.

Ni moja tu ya hukumu za kifo iliyopitishwa na mahakama za sharia nchini Nigeria tangu zilipoanzishwa mwaka 1999.

Mwanamuzi huyo ambaye kwa sasa anashikiliwa mahabusu, alikua amejificha baada ya kutunga wimbo huo.

Waandamanaji walikua wamechoma moto nyumba ya familia yake na kukusanyika nje ya makao makuu ya polisi ya kiislamu huku Hisbah, wakidai hatua ichukuliwe dhidi yake.

Waandamanaji
Maelezo ya picha,Wanaharakati wa Kiislam waliowasihi waandamanaji kutochukua sheria mikononi mwao baada ya wimbo huo kuachiliwa

Wakosoaji wanasema wimbo ulikufuru kwani ulimsifu imam kutoka Waislam wa Tijaniya kiasi kwamba ulimpatia hadhi ya juu kuliko Mtume Muhammad.

‘Hukumu itakua mfano kwa wengine ‘

Kiongozi wa maandamano ambayo yalidai kukamatwa kwa mwanamuziki huyo mwezi Machi, Idris Ibrahim, aliiambia BBC kuwa hukumu itakuwa kama onyo kwa wengine “wanaojaribu kufuata nyayo za Yahaya”.”Niliposikia kuhusu hukumu nilifurahi sanakwasababu inaonesha kuwa maandamano yetu hayakua ya bure.

“Hukumu hii itakua ni mfano kwa wale ambao wanahisi kuwa wanaweza kutukana dini yetu au mtume na waendelee kuwa huru,” alisema.

Yahaya Sharif-Aminu ni nani?

Ni watu wachache ambao waliwahi kumsikia kabla ya kukamatwa mwezi Machi.

Muimbaji huyo wa nyimbo za dini ya kiislamu , hakufahamika sana kaskazini mwa Nigeria na nyimbo zake hazikuwa maarufu nje dhehebu lake la Tjjaniya, kwani kuna wanamuziki wengi wanaoimba kwa kiwango kama chake.

Je hukumu ya kifo hutekelezwa kwa kiwango gani katika mahakama za Sharia?

Hukumu kadhaa zimekuwa zikipitishwa , mkiwemo dhidi ya wanawake wanaopatikana na hatia ya kufanya ngono nje ya ndoa ambazo zililaaniwa sana na kukosolewa kwa kiasi kikubwa.

Lakini ni hukumu moja ambayo imewahi kutekelezwa – dhidi ya mwanaume aliyepatikana na hatia ya kumuua mwanamke na watoto wake wawili ambao waliuliwa kwa kunyongwa mwaka 2002.

Mara ya mwisho mahakama ya sharia ya Nigeria kutoa hukumu ya kifo ilikua ni mwaka 2016 wakati Abdulazeez Inyass, alipohukumiwa kifo kwa kukufuru dini ya kiisalmu baada ya kuendeshwa kwa kesi ya sijri katika jimbo la Kano.

Inadaiwa kuwa alisema kwamba Sheikh Msenegal Ibrahim Niasse, muasisi wa dhehebu la Tijaniya, ambalo lina wafuasi wengi kote Afrika Magharibi , “ni mkubwa kuliko Mtume Mohammad”.

Hukumu haijatekelezwa kwani adhabu ya kifo inahitaji kuidhinishwa kwa saini ya gavana wa jimbo.

line

Ni upi utendaji wa Mahakama za sharia Nigeria?

Mahjimbo kumi na mawili ya yanayokaliwa na waislamu zaidi nchini Nigeria hutumia mfumo wa haki wa sheria ya kiislamu , lakini ni waislamu tu wanaoweza kushitakiwa katika mahakama hizo.

Mfumo wa Sharia , ambao pia una mahakama yake ya rufaa, hushughulikia kesi za kiraia na za uhalifu zinazowahusisha Waislamu na hukumu zake zinaweza pia kupingwa na mahakama za kawaida za Nigeria za rufaa na mahakama ya juu.

Majaji wa Sharia, wanaofahamika zaidi kama alkalis, ni wasomi wa sheria za kiisalamu na sheria za kawaida .

Kama kesi inamuhusu Muislamu na asiye Muislamu, asiye muislamu anaweza kuchagua ni wapi kesi yake itasikilizwa. Mahakama za sharia zinaweza kusikiliza kesi ya asiye Muislamu anapotoa idhini yake kwa maandishi.

Hukumu zinazotolewa na mahakama za kiislamu ni pamoja na kuchapwa viboko, kukatwa viungo vya mwili na kifo.

The post NIGERIA: Mwanamuzi ahukumiwa kifo kwa kumkufuru Mtume Mohammad appeared first on Bongo5.com.