Baada ya serikali kufungua safari za anga la Tanzania,hatimaye ndege ya kwanza ya shirika la ndege la Rwanda imeanza safari zake hapa nchini kwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na abiria kutoka mataifa mbalimbali.

Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Meneja Shirika la ndege la Rwanda hapa nchini Bw. Jimmy Mitali ameeleza faraja yao baada ya kuanza kwa safari hizo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kadico inayosimamia uwanja wa KIA Christina Mwakatobe ameelezea Ujio wa kuanza safari za ndege ya Rwanda hapa nchini umekuwa ni muhimu sana pamoja na ndege nyingine kutoka nchi za ulaya kwani inaonyesha kuwa nchi ni salama haswa katika ugonjwa wa Covid-19.

Fransice Malugu ambaye ni Mwakilishi wa Bodi ya Utalii TTB, amesema kwa sasa mashirika mbali mbali yaliyo kuwa yamesitisha safari zake kwa sasa yameanza kurejesha tena na kwa utalii ni swala zuri na kuwataka wananchi wote kuendelea na utaratibu wa kujikinga na corona.

Chanzo Channel ten.

The post Ndege ya kwanza ya Rwanda yatua Tanzania, baada ya safari za ndege kuruhusiwa nchini appeared first on Bongo5.com.