MWANAMUZIKI wa Afro-Beat, Mnigeria Dare Art Alade ‘Darey’ ameibuka na kusema anatamani kufanya kolabo na wasanii wa Bongo Fleva, akimtaja zaidi Faustina Charles ‘Nandy’ ambaye amekuwa akimkosesha usingizi.

Akizungumza na Gazeti la https://bit.ly/2YDbizu, Darey ambaye alikuwa kimya kwa miaka minne na sasa ameachia wimbo mpya wa Jah Guide Me, amesema akipata nafasi ya kufanya kolabo na wasanii wa Kibongo, atafarijika mno.

“Naweza kusema Afrika ni moja, kwa sasa napambana zaidi kujitanua nje ya Afrika. Najua ili kujijenga pia ndani, natakiwa kushirikiana na wanamuziki wa Afrika Mashariki ambapo muziki wangu unasikilizwa sana.

“Naamini siku nikipata nafasi ya kuimba na Nandy, nitaweza kuweka mizizi zaidi Afrika Mashariki na hasa Tanzania. Kwa kweli wasanii wa Bongo Fleva wanafanya kazi nzuri sana,” amesema Darey.

Darey ambaye ni mtoto wa mwanamuziki mkongwe wa African Jazz, Alade, anamiliki tuzo kadhaa za muziki kama Mwanamuziki Bora, Mwandishi Bora na Mtayarishaji Bora.

STORI: MWANDISHI WETU, DAR