Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara na mgeni rasmi akizinduwa maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, Mkoani Dodoma leo yalioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET). Kulia Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga.
Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga (kulia) akizungumza katika maadhimisho hayo.
Kutoka kushoto ni Afisa Elimu Sekondari Chemba, Valentine Christopher na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara wakiwa meza kuu.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara na mgeni rasmi katika maadhimisho ya Juma la Elimu akipokea begi lenye mchapisho ya maadhimisho hayo kutoka kwa Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga, alipotembelea banda la TENMENT kwenye maadhimisho hayo 
yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, Mkoani Dodoma leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara (kulia) akipata maelezo alipotembelea Banda la TENMET katika maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara (kulia) akipata maelezo alipotembelea Banda la TENMET katika maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara (kulia) akipata maelezo alipotembelea Banda la UWEZO katika maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma. Katikati ni Mratibu wa Uwezo Mkoa wa Dodoma, Nason Nason akifuatilia,
Mratibu wa Uwezo Mkoa wa Dodoma, Nason Nason (katikati) akimuonesha moja ya machapisho yao Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara (kulia) alipotembelea Banda la UWEZO katika maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara (kushoto) akipokea maandamano kwenye maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara (kushoto) akipokea maandamano kwenye maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Bendi ya matarumbeta ikiongoza msafara wa maandamano kwenye maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Maandamano ya wanafunzi kwenye maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Maandamano ya wanafunzi wakiwa na mabango ya jumbe mbalimbali kwenye maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Maandamano ya wanafunzi wakiwa na mabango ya jumbe mbalimbali kwenye maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika wilayani Chemba, mkoani Dodoma.
Maandamano ya wanafunzi kwenye maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara alipotembelea Banda la Watoto Wetu Tunu Yetu-Dodoma katika maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara alipotembelea Banda la HakiElimu katika maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.


Na Joachim Mushi, Chemba
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara ameupongeza Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) kwa jitihada inazozifanya pamoja na wanachama wake kwa kuiunga mkono Serikali hasa katika sekta ya elimu kushirikiana tutatua baadhi ya changamoto za elimu.

Naibu Waziri Waitara ameyasema hayo leo wilayani Chemba alipokuwa akizinduwa maadhimisho ya Juma la Elimu mwaka huu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, ikiwa ni kuleta chachu ya uwajibikaji kwenye sekt ya elimu kwa familia za wafugaji na jamii.

Alisema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ilipoingia madarakani ilibaini kuna kundi ambalo la watu wasiojiweza walikosa elimu kutokana na changamoto mbalimbali za uchangiaji, hivyo iliamua kuja na mfumo wa kutoa elimu bila ada. 

"...Kulikuwa kuna watoto walishindwa kwenda shule, hivyo Rais John Pombe Magufuli akaamua elimu kuanzia ya awali mpaka kidato cha nne iwe bure, kwa maana kwamba elimu bila ada. Hii ndio inaitwa elimu msingi bila malipo. Maamuzi hayo yalipata mafanikio makubwa kwani iliongeza uandikishaji na ufaulu,"

"..Uandikishaji ulipanda kutoka watoto milioni 10 hadi milioni 12 hili ni jambo kubwa na tunampongeza mheshimiwa Rais Magufuli kwa kuliona hilo, maana wapo vijana ambao walikuwa mtaani lakini sasa walienda shule na kuendelea na masomo kidato cha nne hadi cha sita, na pia wengine wameenda hadi vyuo," alisema Waitara na kuongez kuwa Serikali inatumika takribani bilioni 24 kila mwaka kwa ajili ya kuwezesha mpango huo wa serikali. 

Aliongeza kuwa baadaye mwongozo ulitoka wa waraka namba tatu wa mwaka 2016 ulioonesha namna ambavyo jamii inashirikishwa kuchangia kutatua changamoto ndogondogo kwenye elimu ili kuboresha zaidi. 

Alisema Serikali licha ya kutoa elimu bila malipo haijafanikiwa kutoa chakula kwa shule zote, hivyo imeelekeza wazazi wanaweza kujipanga na kuchangia chakula ili mtoto aweze kujifunza huku akipata mlo jambo ambalo linaweza hata kumfanya akaweza kushiriki kikamilifu kupokea mafunzo toka kwa walimu. 

Pamoja na hayo, alibainisha kumekuwa na wazazi ambao wamekuwa hawaupokei vizuri mpango huo wa kuchangi na ndio maana yapo mashirika yanajitolea kusaidia suala hilo, na hata nyie (TENMENT) nimeona mkihamasisha wazazi kujitokeza kuchangia ili kupunguza changamoto katika sekta hii. Lazima tuelewe kuwa hawa watoto ni wakwetu, shule ni za kwetu na nijukumu la jamii kusaidia watoto wetu.

Aidha alisema jambo lingine ambalo linajitokeza kwa sasa ni wazazi kujiweka pembeni kwenye ufuatiliaji taarifa za mtoto wake awapo shuleni, wapo wazazi ambao wakishapeleka mtoto shule wao hujivua kabisa kufuatilia taarifa za mtoto na mwishoni wanajitokeza kumlaumu mwalimu pale mtoto anapofeli mtihani wa mwisho hili sio sawa wazazi lazima tubadilike tufuatilie elimu ya watoto wetu.

Naye Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga alisema maadhimisho ya mwaka huu yamelenga kuhamasisha uelewa wa jamii juu ya haki ya kupata elimu, kuongeza uhamasishaji kwa jamii juu ya uwajibikaji wa pamoja wa elimu na kuhamasisha Serikali kuzingatia na watoto wenye uhitaji, ikiwemo miundombinu ya shule, vifaa vya mafunzo na mafunzo ya ualimu.

Amebainisha kuwa kutokana na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu, Serikali haipaswi kuachiwa kila kitu hivyo wadau wanakila sababu ya kujitokeza na kushiriki kuchangia masuala mbalimbali kwenye sekta hiyo kusaidia kutatua baadhi ya changamoto. 

Katika maadhimisho hayo yalioambatana na maonesho ya shughuli za wanachama wa TENMET, yatashirikisha uchangiaji wa gharama za ujenzi wa bweni la wanafunzi katika Shule ya Sekondari Kwamtoro iliyopo Wilaya ya Chemba. 

Maadhimisho hayo yanaofikia tamati Agosti 21 yataambatana na mijadala mbalimbali, midahalo, ushiriki katika utoaji wa elimu kupitia vyombo vya habari juu ya masuala anuai ya elimu na changamoto zake kwa ujumla.