Aliacha ujumbe mrefu kubainisha chanzo cha kujiua. Picha: Hisani
Caleb alikunywa sumu siku mbili baada ya kurudi kutoka Nairobi alikoenda kumtembelea mkewe

Mkewe aliomba talaka akidai kuwa mimba aliyobeba si yake

Aliacha ujumbe mrefu kubainisha chanzo cha kujiua

Huku janga la corona likizidi kuangamiza familia nyingi, katika familia nyingine, tofauti za kinyumbani zinazidi kuzua vifo.

Caleb, mwalimu katika kaunti ya Kakamega ameamua kujitia kitanzi baada ya kutofautiana na mkewe.

Katika kisa hicho kilichofanyika Alhamisi, Agosti 6, mwalimu huyo anadaiwa kumtembelea mkewe mjini Nairobi alikokuwa akifanya kazi

na kurudi Kakamega siku mbili baadaye.

Kulingana na Peter ambaye alikuwa rafiki yake wa karibu, Caleb alirudi kutona Nairobi baada ya kukosana na mkewe.

Nirbhaya convicts didn't bathe, skipped breakfast before hanging ...

Kulingana naye, mkewe huyo ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi saba alimuomba talaka akidai kuwa mtoto huyo hakuwa wake.

Inadaiwa kuwa suala hilo limuumiza Caleb na kumsukuma kurudi nyumbani haraka licha kuwa shule zimefungwa.

Inadaiwa kuwa mwalimu huyo alijitilia sumu kwenye glasi ya sharubati akainywa na kupatikana kwenye kochi akiwa amefariki.

Maafisa wa polisi waliofika eneo hilo walichukua karatasi ya ujumbe aliyomwandikia mkewe akimtakia maisha mema na marefu.