Bondia Hassan Mwakinyo amefanikiwa kuibuka Bingwa wa mkanda wa WBF baada ya kumpiga kwa point Tshibangu Kayembe wa Congo DR katika pambano la round 12

“Ningecheza mchezo wangu ambao watu wamenizoea nao, ningeweza kushinda ‘knock out’ lakini ingekuwa haina ladha na mara ya mwisho watu walibeza sana ushindi wangu ni kwa sababu nilipigana sikufanya boxing lakini leo niliamua kucheza ndondi...na ndondi inapanda thamani Tanzania kwa sababu yangu...” - Hassan Mwakinyo