MARA baada ya kufungua akaunti yake ya mabao katika klabu yake mpya, kiungo mshambuliaji mpya wa Simba, Bernard Morrison, amefunguka kwamba atazidi kuonyesha uwezo uwanjani kwa kuwa ndipo akili yake ilipo kwa sasa.


 


Morrison aliyetua Simba akitokea Yanga, alifunga bao moja katika ushindi wa mabao 6-0 walioupata Simba dhidi ya Vital’O katika mechi ya Simba Day iliyopigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.


 


Kiungo huyo raia wa Ghana, ameliambia Championi kuwa kwa sasa anaangalia zaidi namna ya kuendelea kuonyesha uwezo wake akiwa uwanjani kwa sababu ndipo akili yake ilipo kwa sasa.


 


“Kuhusiana na mechi hii na Vital’O ilikuwa ni mechi ya kirafi ki na mechi ya maandalizi kabla ya kuanza kwa ligi na tumeonyesha kile ambacho tunajifunza tukiwa uwanjani. Lakini zaidi tumetambulisha wachezaji wapya na hata wale wa zamani.


 


“Kwa sasa nataka niongee zaidi nikiwa uwanjani kwa sababu ndiyo akili yangu ilipo.


Siwezi kuzungumzia sana kuhusiana na mambo ya ligi, ila naangalia kile ambacho kilicho mbele yetu,” alimaliza Morrison.