MCHEZAJI mpya wa Simba raia wa Ghana, Bernard Morrison amepigiwa shangwe kama lote na mashabiki wa Simba mara baada ya kuingia uwanjani alipotambulishwa na Ofisa habari wa Simba, Haji Manara.

Baada ya kupanda katika jukwaa, Morrison alionekana kutembea kwa miguu na mikono kama ambavyo alifanya baada ya kuwafunga Simba akiwa Yanga huku mashabiki wakimshangilia kisha kuchukua kipaza sauti na kuanza kuongea.


“Naipenda Simba. Simba ni chuo cha mpira hapa Tanzania….” Mara baada ya hapo Morrison alianza kucheza nyimbo aliyokuwa inapigwa jambo ambao liliibua shangwe lingine kwa mashabiki. Baada ya utambulisho wa Morrison kumalizika alifuata kiungo Mzambia, Clatous Chama ambaye ndio alikuwa wa mwisho.

Chama baada ya kupanda katika jukwaani, Manara alimfata na kumfunga kamba za vitu na kumbusu miguu yake.

Tukio hilo la Manara kumfunga kamba za viatu Chama linakuwa la pili baada ya kufanya hivyo mara ya kwanza nchini Zambia, katika mazoezi ya mwisho siku moja kabla ya kucheza na Nkana katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka juzi.