Chama cha ACT-Wazalendo, kinatarajia kuwatangaza wagombea wake wa urais wa Muungano na Zanzibar keshokutwa Jumatano

Akizungumza waandishi vya habari jijini Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa Idara ya Habari na Uenezi wa chama hicho, Janeth Rithe, alisema Kamati Kuu ilikutana jana kuyachambua majina hayo.

Alisema Halmashauri Kuu itakutana leo ikifuatiwa na Mkutano Mkuu, yote ikiwa na lengo la kutangaza ilani ya chama na wagombea urais kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.