Imekua ikiaminika kwamba chaguo (Choices) tunayochagua ndio yanatueleza tulivyo. Kuna msemo kwenye Biolojia unasema " Every major decision made human brain undergo a physical change over time" Lakini vipi kuhusu maamuzi ya mtu kuchagua maisha ya kua muuaji?
Watu waliochagua kuishi kama wauaji wapo na huyu ni muuaji wa kutoka Brazili ambaye amekua akifanya uuaji kwa muda mrefu sasa.

Pedro Redrigues Filho ni mmoja kati ya wauaji bora wa muda mrefu lakini yeye uuwaji wake ulikua tofauti na Wauwaji wengine (Killers). Yeye alikua anaua wauaji na wahalifu tu. Anaelezewa kama mmoja wa wagonjwa wa akili (Psychopath) na mchambuzi aliyekua anashughulikia kesi yake.
Amezaliwa katiko mji wa Minas Geraismwaka 1954. Filho alikua na maisha yaliyogubikwa na mateso pamoja na vifo. Filho maisha yake ya unyanywasaji yalianza toka akiwa tumboni kwa mama yake ambapo baba yake alikua akimtesa sana mama yake japokuwa alikua na ujauzito, mateso yalipelekea Filho akapata Damage kwenye fuvu la kichwa chake.
Kutokana na kukulia katika maisha yenye mateso,maumivu na matatizo mbalimbali Filho aliweza kujifunza jinsi ya kujieleza alipokua na miaka 14.

Mtu wa kwanza kuuwawa na Filho alikua mtu aliyemfukuza baba yake kazini.
Baba yake na filho alidaiwa (singiziwa) kuwa ameiba chakula hivyo Naibu meya wa jiji akamfukuza kazi kama adhabu ya wizi. Filho alipopata habari hiyo alikasirika akachukua Bastora akamuua meya mbele ya ukumbi wa jiji, lakini pia filho hakuishia hapo alijua baba yake sio muhalifu (mwizi) hivyo alianza kumtafuta mwizi aliyeiba chakula. Alipomkamata hakumpeleka kwenye vyombo vya dola bali alimuua
Baada ya Filho kufanya tukio hilo ikabidi akimbie mji, alikimbilia eneo la Migi das Cruzes jijini Sao Paul, huku akanguka penzini kwa mara ya kwanza. Lakini huko pia alifanya pia mauaji ya mtu aliyekua anajihusisha na madawa ya kulevya pamoja na kuiba kwenye nyumba za watu.
Mpenzi wake huyo wa kwanza Maria Aparecida Olympia aliuwawa na kikundi kimoja cha wahuni kipindi hiki alikua hajafikisha miaka 18.
Kifo cha mpenzi wake Olympia kilimfanya aamue kuwatesa na kuwaua watu wote walioshiriki kumuua mpenzi wake. Alilipiza kisasi cha mpenzi wake akiwa mwenyewe pekee, kabla ya kufikisha miaka 18 alikua ashaua watu 10.

Filho alikua maarufu zaidi alipolipiza kisasi juu ya kifo cha mama yake mzazi. Na mlengwa alikua baba yeke mwenyewe ambaye alimuua mama yake filho kwa kumkata kata na mapanga. Iikua hivi
Filho alimtembelea gerezani baba yake ambapo alimchoma na visu mara 22 kisha akachomoa moyo wa baba yake na kuutafuna.

Pia siku moja alikua njiani ndani ya gari la polisi anasafirishwa akiwa na mtu mwingine ambaye alikua anatuhumiwa kwa makosa ya Ubakaji, filho alimua mule mule ndani ya gari la polisi na polisi wakiwemo. Hapo ndipo alipoanza kua muuaji wa wauaji (The killer of killers)
Kaua wauaji 47 aliokua kafungwa nao gerezani. Moja kati ya Mahojiano yake alisema "Thrill and joy out of killing other criminals"
Siraha yake aliyokua akiipenda kutekeleza mauaji ni upanga.

Japo alifanya mauaji mengi bwana Filho aliachiwa huru, alikua amehukumiwakifungo cha miaka 128 japokua sheria za Brazil haziruhusu mfungwa kufungwa zaidi ya miaka 30. Aliachiwa mwaka 2007 lakini aliahidi kuwaua waharifu wote nchini Brazil.
Mwisho
Tchao.