Janga la virusi vya Corona vimeathiri karibia kila taifa duniani isipokuwa mataifa haya 10. Swali la kujiuliza yanafanya nini mataifa hayo?

People of Micronesia | Micronesia, Federated states of micronesia ...

Watu wa taifa la Micronesia

Hoteli ya Palau ni maarufu kwasababu ilipofunguliwa 1982 ilikuwa hoteli ya pekee kwani hakukuwepo na hoteli nyengine.

Tangu wakati huo taifa hilo dogo, linalozungukwa na bahari ya pacific limejipatia watalii wengi. Mwaka 2019 , watalii 90,000 walitembelea Palau , ikiwa ni idadi mara tano ya jumla ya idadi iliopo.

2018 Micronesia Island Fair Coming Up - Discover the South Pacific

Watu wa taifa la Micronesia

Mwaka 2017, takwimu za IMF zilionesha kwamba utalii ulichangia asilimia 40 ya kipato cha nchi hiyo cha kila mwaka. Lakini hilo ni kabla ya mlipuko wa virusi vya corona kuanza.

Mipaka ya Palau ilifungwa tangu mwisho wa mwezi Machi. Ni miongoni mwa mataifa 10 duniani ambayo hayakuthibitsha mgonjwa yeyote wa Covid 19 bila kuorodhesha Korea kaskazini na Turkmenistan.

Hoteli hiyo ya Palau imefungwa tangu mwezi Machi na haipo pekee.Wakaazi wakisaidia meli ya watalii katika kisiwa cha Vanuatu mwezi Disemba 2019 sula ambalo haliwezi kufanyika wakati ambapo mipaka imefungwa

Migahawa haina watu, maduka yamefungwa na wageni wa pekee ni raia waliojiweka katika karantini.

Mataifa ambayo hayajathibitisha hata mgonjwa mmoja wa corona.

  • Palau
  • Micronesia
  • Marshall Islands
  • Nauru
  • Kiribati
  • Solomon Islands
  • Tuvalu
  • Samoa
  • Vanuatu
  • Tonga

Bahari hapa ni nzuri na yenye mandhari ya kuvutia zaidi ya eneo lolote lile jingine duniani, kulingana na Brian Lee, meneja na mmiliki mwenza wa hoteli ya Palau.

Ni bahari ya rangi ya bluu ambayo ilimfanya Brian kuwa na kazi ya kufanya. Kabla ya Covid 19 vyumba vyake 54 vilikuwa na kati ya asilimi 70 na 80 ya wageni , lakini mipaka ilipofungwa , hakukuwa na chengine cha kufanya.

”Ni taifa dogo , hivyobasi wakaazi hawawezi kuishi Palau”, anasema Brian.Visiwa vya bahari ya pacific havikuandikisha mgonjwa yeyeote wa corona

 

Ana takriban wafanyakazi 20 na amefanikiwa kutowafuta kazi huku wakifanya kazi kwa saa chache .

”Najaribu kuwatafutia kazi, kupitia kufanya ukarabati na kadhalika”, anasema. Lakini hoteli zisizo na wateja haziwezi kukarabatiwa kila siku .

Nitaendelea kutoa huduma kwa nusu mwaka mwengine halafu nifunge , anasema Brian.

Briana hailaumu serikali, ambayo imetoa usaidizi wa kifedha kwa raia wake mbali na kufanikiwa kuzuia kuingia kwa virusi hivyo.

The post Mataifa 10 ambayo hayajathibitisha hata mgonjwa mmoja wa CORONA appeared first on Bongo5.com.