Vyombo vya habari vya China vinaripoti kuwa mwasisi wa kampuni ya teknolojia ya Bytedance ambayo ndiyo mmilki wa mtandao wa kijamii wa Tik Tok, amesema leo kuwa wanafanya jitihada kuhakikisha kuwa wanapata matokeo mazuri, wakati ambapo mazungumzo yanaendelea kuhusiana na kuuzwa kwa operesheni zake za Marekani kwa kampuni ya Microsoft.

Tik Tok ambayo ni maarufu sana miongoni mwa vijana Marekani na kote duniani ndio mtandao wa hivi karibuni unaolengwa katika mzozo wa kibiashara kati ya China na Marekani.

Marekani imesema kampuni hiyo inayomilikiwa na Mchina, ni kitisho cha usalama wa kitaifa, jambo ambalo Tik Tok inakanusha.

Microsoft imesema kwamba itaendelea na mazungumzo ya kununua operesheni Tik Tok Marekani. Tik Tok inakadiriwa kuwa na watumiaji bilioni moja kote duniani.
KWA HABARI, LIVE